Polisi Mkoa wa Simiyu wanamshikilia mtu mmoja, Emmanuel Sulwa Mapana (24), maarufu kwa jina Mchambi, akiwa na sare za Jeshi la Wananchi Tanzania zenye cheo cha luteni.
Taarifa ya Jeshi hilo iliyotolewa na Kamanda wa Polisi, imeeleza kuwa tukio hilo limetokea hii leo Januari 14, 2025 majira ya saa 6:30 mchana ambapo mtu huyo alikamatwa akiwa amevaa Kombati hizo.
![](https://jambofm.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250214-WA0064-1024x693.jpg)
“Alikuwa na gari aina ya Ractic yenye namba ya usajili T 560 DCS na mara baada ya kufanyiwa upekuzi alikutwa na Mkanda wa Jeshi la Wananchi na Laptop moja,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Polisi wanaeleza kuwa, Emmanuel Sulwa Mapana ambaye ni Mkazi wa Mtaa wa Sima, Wilaya ya Bariadi Mkoa wa Simiyu, alikuwa akitafutwa kwa kipindi kirefu kwa kosa la kujifanya mtumishi wa serikali.