Atletico Madrid wanatafakari uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Nicolas Jackson msimu wa joto, huku Aston Villa na Newcastle pia zikimfuatilia mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal, 23. (Sun)
Paris St-Germain wanavutiwa na beki wa Liverpool mwenye umri wa miaka 25 wa Ufaransa Ibrahima Konate, ambaye yuko tayari kuhamia Ligue 1. (ESPN)
Newcastle imeungana na Brentford na Brighton katika kinyang’anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Celtic Mjerumani Nicolas Kuhn, 25. (Team Talk)
Manchester City imeungana na vinara Bayern Munich katika mbio za kumsajili kiungo mshambuliaji wa Ujerumani Florian Wirtz, 21 kutoka Bayer Leverkusen. (Football Insider)
Chelsea imefanya mawasiliano na wawakilishi wa kiungo wa kati wa Barcelona na Uhispania Marc Casado mwenye umri wa miaka 21 kuhusu uwezekano wa kumsajili mchezaji huyo. (Cadena SER – kwa Kihispania)
Winga wa Athletic Bilbao Mhispania Nico Williams, 22, anaihusudu Barcelona, licha ya kuwindwa klabu za Arsenal na Liverpool za Ligi ya Premia. (TBR Football)