Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, linawashikilia Vijana zaidi ya 100 kwa tuhuma za kujihusisha na biashara inayoendana na upatu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Februari 15, 2025 mjini Mlandizi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Salimu Morcase amesema wanaendelea kuwafanyia mahojiano zaidi, ili kubaini kiundani.

Amesema, “tumewakamata katika maeneo matatu tofauti hapa Mlandizi na wanatoka Mikoa mbalimbali biashara wanazozifanya hazieleweki na zinaendana na upatu.”

Kamanda Morcase amesema mahojiano ya awali yanaonesha Vijana hao wamekuwa wakiitana kutoka mikoa mbalimbali huku wakiaminishana kuwa huku waliko wana maisha mazuri jambo ambalo halina ukweli.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Salimu Morcase akizungumza kwenye eneo la tukio Mlandizi Kibaha Mkoa wa Pwani.

“Wanasema wananunua bidhaa kisha wanazitumia na ili wapate faida wanatakiwa
Kutafuta watu wapya na kuwaingiza kwenye mfumo wao. Tunaendelea kuwafanyia mahojiano na baadae watachukua hatua stahiki kulingana na sheria zinavyoagiza,”

Kamanda Morcase amesema wanaendelea kuwafanyia mahojiano na baadaye watachukua hatua stahiki kulingana na sheria zinavyoagiza.

Simba na Yanga acheni porojo angalieni anayofanya Al Ahly
Safari ya Jackson kwenda Hispania imewadia