Afarah suleiman, Mbulu – Manyara.

Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, imekabidhi jumla ya pikipiki 16 za mikopo ya asilimia 10 kwa makundi matatu ya Vijana katika Halmashauri hiyo yenye thamani ya jumla shilingi million 45,935,000 ili kuwawezesha vijana hao kujikwamua kiuchumi.

Akikabidhi Pikipiki hizo, Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Michael John Semindu amewataka vijana wanufaika wa mikopo hiyo kuweza kurejesha Kwa wakati ili vijana wengine waweze kunufaika na mikopo hiyo ya asilimia kumi ya Halmashauri.

Naye Mbunge wa mbulu Vijijini, Flatei Gregory ametoa msisitizo kwa vVijana na wanawake Kujitokeza Katika fursa mbalimbali zinazo jitokeza ili waweze kunufaika na kujikwamua kiuchumi na Kuleta maendeleo Katika jamii yao.

Aidha mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Abubakari Kuuli na mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbulu, Joseph Mandoo amesema mikopo hiyo ya asilimia 10 itaendelea kutolewa Kwa makundi hayo ya Vijana pamoja na Wanawake, hivyo ni vyema ikarudishwa kwa wakati.

Baadhi ya Vijana walionufaika na mkopo huo ambao ni kati ya shillingi 204,635,000 zilizokopeshwa na Halmashauri hiyo wameishukuru Serikali kwa fursa ya mikopo isiyo na riba, ambayo inawakomboa kiuchumi.

Katika hatua nyingine Halmashauri hiyo imekabidhi jumla vitambulisho vya utambuzi kwa wajasiriamali 52, kwa awamu ya kwanza.

Wanahabari watakiwa kutumia vizuri Kalamu zao
Simba na Yanga acheni porojo angalieni anayofanya Al Ahly