Naibu waziri wa habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma amewaasa Waandishi wa Habari Nchini kutoiporomosha Demokrasia kutokana na kazi ya kalamu zao, hasa kipindi hiki ambacho Nchi inaelekea kwenye uchaguzi mkuu.
Mwinjuma ametoa kauli hiyo leo Februari 14, 2025 hapa Jijini Dodoma wakati akifunga kikao cha siku mbili cha Waandishi wa Habari Nchini amba katika maadhimisho ya Siku ya Utangazaji Nchini ambapo amewataka Waandishi kuwa makini na Teknolonia ya akili unde ambayo imitumika vibaya inaweza kuwa matokeo hasi kwa jamii kipindi cha uchaguzi.
Amesema, kupitia mafunzo hayo anaamini Waandishi wamejifunza mambo mbalimbali ya kitaaluma, na kwamba yamewajenga hasa kwenye utoaji wa taarifa sahihi hasa katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa 2025.
![](https://jambofm.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/Screenshot_20250215-054813_Gmail.jpg)
“Vyombo vya habari ni muhimu sana kuelekea kwenye uchaguzi kuu wa mwaka huu, na msipotoa taarifa sahihi mnaweza kuchangia demokrasia kuzama,” amesema Mwinjuma.
“Hivyo nawasihi mtoe taarifa sahihi, zisizoegemea upande wowote, na mhabarishe umma ili wafanye machaguo sahihi kwa kuchagua viongozi wanaowataka,” ameongeza.
![](https://jambofm.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/Screenshot_20250215-054921_Gmail.jpg)
Amesisitiza pia suala la matumizi ya lugha sahihi ya kiswahili katika utangazaji, ili kuilinda lugha hiyo na kutokubali kuharibiwa, bali waitumie kwa ufasaha.
Aidha, amesema serikali ipo pamoja na sekta ya Habari, na kwamba milango ya Wizara ipo wazi, na kusisitiza dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassani ni kuikuza Sekta hiyo na ndiyo maana alipoingia Madarakani alivifungilia vyombo vya habari ambavyo vilikuwa vimefungiwa.
![](https://jambofm.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/Screenshot_20250215-054842_Gmail.jpg)
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), Mhandisi Andrew Kisaka naye amesisitiza Waandishi wa Habari kuwa makini wanapo ripoti habari za uchaguzi na kutoongeza “Chumvi”, pamoja na kutoa uwiano sawa wa muda wa vipindi kwa Wagombea.
Amesema mikutano hiyo wameianzisha TCRA, kwa malengo ya kukuza sekta ya utangazaji.
Zaidi ya wanatasnia ya Habari 500 wamehudhuria kikao hicho ambacho kimebebwa na kauli mbiu ya Wajibu wa Vyombo vya Utangazaji kuelekea Uchaguzi wa Mwaka 2025.