Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Februari 19, 2025 atazindua kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia katika mkoa wa Lindi, kwenye viwanja vya Madini, Ruangwa Mkoani humo.

Lengo la Kampeni hiyo, ni kuwafikia wananchi wenye uhitaji na wasio na uwezo wa kumudu gharama za huduma za kisheria. Pia kampeni hiyo itawezesha kupata utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala, kuongeza uwajibikaji kwa watendaji na kuimarisha umoja na mtangamano miongoni mwa jamii.

Mpaka sasa kampeni hiyo imefika katika mikoa 16 na kuhudumia wananchi zaidi ya milioni 1 na Kaulimbiu ni “Msaada wa Kisheria kwa Haki, Usawa Amani na Maendeleo”.

Dkt. Biteko ampongeza Mwanafunzi aliyeelezea Miradi ya Umeme
Viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji wajengewe uwezo - Katimba