Chebukati amefariki katika Nairobi Hospital baada ya kuugua kwa muda mrefu na kifo chake kimethibitishwa na Rais wa Kenya, William Ruto. Tarifa zinadai kuwa, Chebukati alifariki majira ya saa tano usiku wa kuamkia siku ya leo Ijumaa ya Februari 21, 2025 wakatia akiwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali moja jijini Nairobi.
Chebukati alihudumu kama Mwenyekiti wa IEBC kwa muhula mzima wa miaka sita na alistaafu Januari 2023, baada ya kuongoza Uchaguzi Mkuu wa 2017 na 2022. Wakati wa uongozi wake, alisimamia chaguzi tatu za Kenya, ukiwemo uchaguzi mkuu wa 2017, uchaguzi wa marudio wa urais wa Oktoba 2017 na uchaguzi mkuu wa 2022.
Enzi za uhai wake, Chebukati alikuwa pia ni Wakili mzoefu kwa miaka 37 na aliendesha kampuni yake ya uanasheria kwa zaidi ya miaka 20 ambapo mwaka 2006, alianzisha kampuni ya uwakili ya Cootow & Associate Advocates, aliyoachana nayo Januari 17, 2017, kisha kuwa mwenyekiti wa IEBC.

Serikali kuwafikia Vijana utoaji wa Elimu tahadhari ya UKIMWI
Tanzania, Comoro wazungumzia ushirikiano sekta ya uwekezaji