Uwepo wa Migogoro ya Ardhi Wilayani Handeni, umepelekea Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius Ndejembi kumuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhandisi Anthony Sanga kumsimamisha kazi na kumchukulia hatua za kinidhamu Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Mji Handeni.

Ndejembi ametoa agizo hilo alipofanya ziara katika Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga ambapo alitembelea eneo la Kwanjugo Kitalu A, ambaloWananchi wake wamekua wakilalamika kwa muda mrefu kuchukuliwa maeneo yao, bila kulipwa fidia.

Amesema, “kiasili pana historia yake, palikua pana umiliki wa wenyewe sasa haiwezekani watu hawa kuonewa, na migogoro yote hii ni kwa sababu hatusikilizi wananchi wetu, sasa ninamuelekeza Katibu Mkuu kumsimamisha mara moja Mkuu wa Idara ya Ardhi wa Halmashauri na haraka sana aletwe mtu mwingine atakayeweza kutatua migogoro ya ardhi Handeni.”

Ndejembi ameongeza kuwa, “Lninaelekeza kuundwa kwa Timu ya uchunguzi itakayokua chini ya Kamishna wa Ardhi, ije hapa Handeni ndani ya wiki moja ili ichunguze umiliki wa viwanja vya sasa ni akina nani, na kama ni watumishi wa ardhi tuchukue hatua kali. Kwa sababu hatuwezi kuruhusu watumishi wa ardhi kunyang’anya ardhi ya wananchi.”

Aliyewajibu isivyo Watumishi wa Serikali achukuliwa hatua
Serikali kuwafikia Vijana utoaji wa Elimu tahadhari ya UKIMWI