Mshambuliaji Waziri Junior leo ameanza safari ya kwenda kujiunga na klabu yake mpya ya Al Mina’a inayoshiriki Ligi Kuu nchini Iraki.
Meneja wa mshambuliaji huyo, Thomas Ng’itu amesema kilichokuwa kinamchelewesha mteja wake kuondoka kwa wakati ni Visa.
“Visa ndio ilikuwa changamoto kwani Al Mina’a ndio walikuwa wanashughulikia kila kitu, utaratibu wa nchi (Iraki) muda mwingine huchukua hadi mwezi kupata visa;
“Hivyo wamepambana na juzi ilipatikana, jana wakatuma tiketi na leo ameondoka.”
Junior amejiunga na timu hiyo kwa mkopo wa miezi sita akitokea klabu ya Dodoma Jiji inayoshiriki Ligi Kuu nchini.