Kocha wa Manchester United, Ruben Amorim, amewataka viongozi wa klabu hiyo kumsajili winga wa timu ya vijana ya Ureno chini ya miaka 21, Geovany Quenda, mwenye umri wa miaka 17, kutoka klabu yake ya zamani Sporting kwa dau la pauni milioni 35 (Star)
West Ham wana nia ya kumsajili beki wa kati wa Southampton, Taylor Harwood-Bellis, mwenye umri wa miaka 23 na anayewakilisha timu ya taifa ya England (Sun – subscription required)
Real Madrid bado wanamtaka Jarrad Branthwaite lakini wanasita kutoa dau la pauni milioni 62 wanalotaka Everton kwa ajili ya kumuuza beki huyo wa kati wa England mwenye umri wa miaka 22. (Diario AS – in Spanish)
Crystal Palace wanavutiwa na usajili wa mshambuliaji wa Liverpool, Lewis Koumas, mwenye umri wa miaka 19 na anayeichezea Wales, pamoja na winga wa Scotland mwenye umri wa miaka 19, Ben Doak, ambao kwa sasa wako kwa mkopo katika timu za Stoke na Middlesbrough, mtawalia. (Alan Nixon)
Real Madrid wanataka kumbakiza Luka Modric na wako tayari kumpa kiungo huyo wa Croatia, ambaye atatimiza miaka 40 mwezi Septemba, mkataba mpya. (Nicolo Schira)
Tottenham wako tayari kumuuza Manor Solomon msimu huu wa kiangazi, huku Leeds, ambako winga huyo wa Israel mwenye umri wa miaka 25 yuko kwa mkopo pamoja na Everton wakionesha nia ya kutaka kumsajili. (Givemesport)
Liverpool wanatumai kuwashinda Arsenal katika umsajili wa kiungo kinda wa Rosenborg, Sverre Nypan, mwenye umri wa miaka 18 na anayechezea timu ya taifa ya Norway chini ya miaka 21. (Fichajes – in Spanish)