Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amesema yuko tayari kujiuzuru urais wake ili kufanikisha amani, huku Ukraine ikitimiza miaka mitatu tangu kuvamiwa rasmi na Urusi, Februari 24, 2025.

Kauli hiyo ya Zelensky imekuja baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kumuita Zelensky Dikteta licha ya kudai kuwa kauli hiyo haikumpa maudhi kwani yeye si Dikteta kama anavyosema kwani alichaguliwa kidemokrasia mnamo Mei 2019.

“Iwapo mnahitaji niondoke kwenye kiti hiki, niko tayari kufanya hivyo. Na pia naweza kufanya hivyo ili Ukraine kuwa mwanachama wa NATO, na pia sikuudhika kuitwa dikteta maana Dikteta angeudhika,” alisema rais huyo wa Ukraine.

Zelensky alisema kwa sasa amejikita katika masuala ya usalama wa Ukraine na kwamba si ndoto yake kubaki madarakani kwa muongo mmoja kwani sheria za Ukraine zinakataza kufanyika kwa uchaguzi wakati kukiwa na vita, hali ambayo imekuwepo tangu Urusi ilipoanzisha uvamizi wake Februari 2022.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya na dunia wanatarajiwa kuelekea Kyiv hii leo Februari 24, 2025 kuonesha mshikamano wao kwa Ukraine na kujadili hali ya usalama, huku Waziri Mkuu wa Hispania Pedro Sanchez, Rais wa Baraza la Ulaya Antonio Costa, na Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen wakiwa ni miongoni mwa wanaotarajiwa kushiriki mkutano huo.

Watakiwa kutopandisha bei za Vyakula mwezi Mtukufu
Rais Samia katika hafla ya Uzinduzi wa Jengo la Halmashauri Bumbuli