Saulo Steven – Manyara.
Wazazi na walezi Mkoani Manyara wametakiwa kutumia vikao vya wazazi Mashuleni ili kuwaandikisha wanafunzi waweze kusajiliwa na mfuko wa bima ya Afya NHIF kwa ajili ya kupatiwa matibabu pindi wanapopatwa na changamoto za Afya.
Rai hiyo imetolewa na Maeneja wa Mfuko wa Taifa wa bima ya afya NHIF mkoa wa manyara Emmanuel Mwikwabe wakati akizungumza na Dar24 ofisini kwake kuhusu mpango wa usajili wa wanafunzi na vifurushi vya bima ya Afya kwa shule zote binafsi na serikali kuanzia ngazi ya awali hadi vyuo vikuu.
Amebainisha kuwa kupitia vikao hivyo vitasaidia wazazi na walezi kuweza kuelimishwa juu ya kutambua umuhimu wa bima ya Afya kwa wanafunzi kwani kwa kufanya hivyo wanafunzi watakuwa na uhakika wa kupatiwa huduma ya matibabu kwa kuchangia kiasi cha shilingi elfu hamsini na mianne 50,400/= kwa mwaka.
Mwikwabe amwesihi wazazi na walezi mkoani humo kuacha tabia ya kujificha kwenye mwamvuli wa kutougua na kudhani kwamba wana uwezo wa kumudu gharama za matibabu pindi zinapotokea changamoto za afya kwa watoto jambo ambalo ni gumu hivyo ni muhimu kujiunga na huduma za mfuko wa bima ya Afya ili kuwa na uhakika wa Matibabu.
Sanjari na hayo Meneja huyo wa NHIF mkoa wa Manyara amesisitiza kuwa ili mwanafunzi aweze kuandikishwa katika usajili wa wanafunzi na virushi vya bima ya Afya ni lazima aandikishwe katika shule anayosoma na sivingenevyo ili kuendana na utaratibu uliopangwa kwa mujibu wa Sheria.