Mahakama ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro imemhukumu Juma Rekote Mkandira (44), mkazi wa kijiji cha Kitunduweta – Mhenda Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro kwa kosa la kumlawiti mtoto wa kike wa umri wa miaka saba (jina limehifadhiwa) ambaye ni mwanaye wa kumzaa.

Juma alikamatwa na Jeshi la Polisi januari 18,2025 katika Kijiji cha Kitunduweta na kufikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Kilosa Februari 26, 2025 ili kujibu tuhuma zilizokuwa zinamkabili.

February 26,2025 ,Mbele ya Mh.Ageness Ringo mshitakiwa alikiri kosa na kuhukumiwa kwenda Jela kufungo cha Maisha ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.

TANESCO waendeleza mradi wa Umeme Makambako - Songea
Kesi chapisho la uongo: Dkt. Slaa aachiliwa huru