Kijana David Jegi Lusanja mkazi wa Kata ya Kitangiri iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya  Shinyanga anayekabiliwa na maradhi katika ya kibofu cha mkojo na kushindwa kujisaidia katika hali ya kawaida, anaomba msaada, ili aweze kupata matibabu ambayo gharama yake ni shilingi Milioni 2.

Anatokea katika kijiji cha Kidinda cha Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, na yupo Mkoani Shinyanga kwa Ndugu zake kutafuta msaada huku akisema tatizo hilo lilianza miaka miwili iliyopita baada ya kuangukiwa na kifusi akiwa katika shughuli za uchimbaji wa madini katika mgodi mdogo wa dhahabu wa Dutwa wa Wilayani Bariadi mkoani Simiyu.

David ni mtoto anayetoka kwenye familia duni na anasema kutokana na tatizo hilo kudumu kwa muda murefu, limepelekea utendaji kazi wa figo zake kuanza kuzorota na kwamba anahitaji matibabu ya mapema, ili kunusuru uhai wake.

Alipatiwa rufaa kutoka Hospitali ya Mkoa wa Simiyu, kwenda Hospitali ya Kanda ya Bugando kwa matibabu zaidi ambapo ameainisha kuwa gharama za matibabu yote ni shilingi milioni mbili ambayo yeye pamoja na familia yake hawana uwezo wa kuimudu.

Msamaria mwema yeyote atakayeguswa kuokoa maisha ya kijana David na kutaka kutoa msaada wa matibabu yake ama fedha anaweza  kuchangia fedha au kuwasiliana naye kupitia simu namba 0680408335 ambayo imesajiliwa kwa jina la Willy Mwapili.

Vikundi 60 Wilayani Ilemela vyanufaika na mkopo wa Bilioni 1
Uwezeshwaji umewasaidia Wanawake kuinuka kiuchumi