Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela amesema hadi sasa Sh 1.5 bilioni zimetolewa na Halmashauri za Geita kwenye vikundi 173 na kati ya hivyo vikundi 63 ni vya wanawake.
RC Shigela ameyasema hayo katika kongamano maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani kwa Kanda ya Ziwa, lililofanyika Wilayani Bukombe Mkoani Geita.
Amesema, katika sekta ya madini vikundi 60 vya wanawake vimepatiwa leseni na mwanamke ana nafasi kubwaya kukuza uchumi wa familia kwani ndiye mlezi na Mwalimu wa kwanza.
Akiongea katika Kongamano hilo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, alisema kuna haja ya siku ya Wanaume Duniani ikatambuliwa rasmi kama inavyoadhimishwa siku ya Wanawake, ili waweze kutambua nafasi yao katika kulinda familia.

Upungufu wa Wataalamu unachangia ongezeko la vifo vya Wanawake, Watoto - Salome
Wanaume watambue nafasi zao katika kulinda familia - Dkt. Gwajima