Taarifa kutoka Vatican, imethibitisha kuwa afya ya Papa Francis inaendelea kuimarika baada ya kupitia changamoto ya upumuaji na Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki hahitaji tena mashine ya kusaidia kupumua.
Papa Francis (88), amekuwa akikabiliwa na matatizo ya kiafya ikiwemo maambukizi ya mapafu, ingawa hakuna maelezo ya ziada kuhusu matibabu anayopatiwa.
Waumini na Viongozi wa kidini duniani kote wamekuwa wakifuatilia kwa karibu afya yake huku wakimuombea apone haraka, wakitarajia atarejea tena katika majukumu yake.
Alilazwa katika Hospitali ya Gemelli iliyopo jijini Rome Februari 14, 2025 hadi alipogunduliwa kuwa na maradhi hayo na kuzua taharuki kwa Waumini wa kanisa hilo duniani.

Prof. Mkenda asisitiza umuhimu wa Elimu ya amali kukuza ujuzi
Ifahamu sehemu hatari kwa maisha ya Wanawake Duniani