Waziri wa zamani katika Serikali ya Tanzania na Mbunge wa Rorya, Prof. Philemon Sarungi amefariki dunia leo nyumbani kwake Msasani Jijini Dar es Salaam.

Tarifa ya Msemaji wa familia ya Sarungi, Martin Leonard Obwago imethibitisha kutokea kwa kifo hicho hii leo Machi 5, 2025.

Profesa Sarungi amefariki Majira ya saa 10, jioni na msiba upo nyumbani kwake na taarifa zaidi zitakujia kuhusu utaratibu.

Wanaume kikwazo cha maendeleo ya Wanawake Katavi