Naibu waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Mbunge wa Babati vijijini Daniel Baran Sillo amefanya ziara katika kijiji cha Gidabaghar kata ya Boay ambapo ametoa jumla ya mifuko 100 ya simenti kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya Gidabaghar na jezi kwa ajili ya michezo

Sillo ameelezea utekelezaji wa ilani ya CCM (2020-2025) katika Jimbo la Babati Vijijini ambapo vituo 5 vya afya vimejengwa, Madara zaidi ya 108, zahanati 11 zimepewa milioni 50 Kila Moja na bajeti ya TARURA imepanda toka milioni 600 ahadi bilioni 2.

Sanjari na hayo Sillo alimshukuru Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za maendeleo ambapo zimewezesha kugusa vijiji vyote nchini kwenye miradi tofautitofauti ya afya, maji, umeme, mabarabara, madaraja pamoja na Miundombinu mingine.

AU yaridhia kuongeza matumizi sekta ya ulinzi
Kamati yataka Miundombinu Daraja la Mawe Garkawe ilindwe