Adhabu mbadala kwa wahalifu, zinatarajia kupunguza gharama za kuhudumia wafungwa na kuwapa fursa wahalifu wa makosa madogo madogo kujirekebisha, huku wakiendelea kuchangia maendeleo ya jamii.
Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo wakati wa uzinduzi wa Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii na kudai kuwa utaratibu huo utaimarisha mfumo wa haki jinai Nchini.
Amesema, upo umuhimu wa matumizi ya adhabu hiyo kwa wahalifu wa makosa madogo, badala ya vifungo magerezani, ambayo ni hatua muhimu ya kupunguza msongamano wa wafungwa Gerezani.