Takwimu zinaonesha kuwa kati ya Julai 2021 hadi Februari 2025, jumla ya watalii 2,916,540 wametembelea vivutio vya utalii ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 10, 2025 Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA), Dkt. Elirehema Doriye amesema katika kipindi hicho, mapato ya shilingi 693,959,894,001 yamekusanywa na kuingia kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali.
“Mwaka wa fedha 2021/220 Idadi ya watalii walikuwa 425,386 ambapo Watalii wa nje walikuwa 228,810, Watalii wa ndani 196,576 Mapato yaliyokusanywa TZS 91,131,434,280.54, Mwaka wa fedha 2022/23 Idadi ya watalii 752,232 ikiwa Watalii wa nje 458,351, Watalii wa ndani 293,881
Mapato yaliyokusanywa ni TZS 171,257,737,653.10,” amesema.

“Na Mwaka wa fedha 2023/24
Idadi ya watalii 908,627 ikiwa Watalii wa nje 553,875, na Watalii wa ndani 354,752 Mapato yaliyokusanywa ni TZS 219,547,542,813, vilevile Mwaka wa fedha 2024/25 (Julai – Februari 2025)
Idadi ya watalii 830,295 ikiwa Watalii wa nje 509,610, Watalii wa ndani 320,685
Mapato yaliyokusanywa ni TZS 212,023,179,255.68,” amesema Dkt. Doriye.
Vilevile amesema kwa mwaka 2024/25 mwenendo unaonyesha mamlaka itapata watalii zaidi ya Milioni moja na mapatozaidi ya lengo ambalo iliweka ambalo ni kukusanyaBilioni 230 ambapo hadi sasa katika mapato hayaimeshakusanya asilimia 92.
Hata hivyo, amesema Serikali kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya barabara na maji kwa lengo la kuboresha miundombinu ndani ya hifadhi na maeneo inayoyasimamia.

“Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imefanikiwa kutengeneza mtandao wa barabara wenye urefu wa jumla ya kilomita 173 kwa kiwango cha changarawena kilomita 4.2 kwa kiwango cha tabaka gumu (mawe),Aidha, mamlaka imenunua malori 14 na mitambo ya ujenzi wa barabara ili kuimarisha shughuli za matengenezo na ujenzi ikiwa Jumla ya Shilingi Bilioni 14.993 zilitumika kutekeleza miradi hii ambayo imekamilika kwa asilimia 100%”, amesema
“Hifadhi ya Ngorongoro imefanikiwa kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji ndani ya hifadhi na maeneo inayoyasimamia kupitia ujenzi wa miradi mbalimbali ya maji yenye jumla ya gharama ya TZS 1.5 bilioni.

Miradi hii imekamilika kwa asilimia 100% na inajumuisha Ujenzi wa Mtambo wa Kutibu Maji wa Mama Hhau, Ujenzi wa Tanki la Maji la Lita 135,000 kwenye Mnara wa Mita 6 katika Lango la Loduare, Uchimbaji wa Visima Virefu vya Maji (3) maeneo ya Laetoli, Olduvai na Ndutu na Ujenzi wa Mradi wa Maji katika Kituo cha Kimondo.” Amesema Dkt. Doriye.