Rais Samia Suluhu Hassan amewaeleza wakurugenzi wanaotaka kwenda majimboni kuwania nafasi ya ubunge kutoa taarifa mapema ili waandaliwe waliopo chini yao.
Rais Samia ameyasema hayo leo Jijini Dodoma katika Mkutano wa 39 wa ALAT uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano Jakaya Kikwete Conversion Center ambapo amesema katika kuelekea harakati za uchaguzi, endapo kuna Wakurugenzi wakuu wa Mkoa na wakuu wa Wilaya wanaotaka kuingia majimboni watoe taarifa mapema ili waanze kuandaliwa waliopo chini yao kwa lengo la kuwapandisha vyeo badala ya wateule hao kuondoka na kusabaisha teuzi kuwa ngumu.
“Kwa sasa tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu kama kuna wakurugenzi,wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wanaotaka kwenda kugombea watoe nafasi mapema ili tuanze kuwatengeneza waliopo chini yao kushika nafasi hizo ”amesema.
“Kuna wakati unakuta watu wote wanaondoka kwenda kuchukua fomu na kuziacha ofisi hazina watendaji kutokana na hali hiyo inapelekea kuteua watu ambao hawana uzoefu jambo ambalo siyo sahihi, Kama mtu anataka kwenda kuchukua fomu ni lazima kujipima na kutoa taarifa iwapo haukutoa taarifa unaweza kujikuta unakosa yote maana unaweza kukosa huko na huku ukakuta nafasi yako imejazwa lakini kama utatoa taarifa na ulikuwa mtendaji mzuri unaweza kufikiriwa”. Amesema Dkt. Samia
Hata hivyo amesema “Watu wanaokwenda kugombea ni watu ambao tayari wamejipanga na wana uwezo wa kuendesha gurudumu la maendeleo na siyo watu ambao hawajajiaandaa,”amesema
Vilevile amezitaka halmashauri kuhakikisha inasimamia mapato yanayokusanywa katika halmashauri zao kwa lengo la kufanikisha maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.