Taarifa kutoka Nchini Ukraine, zinaarifu kuwa Taifa hilo limekubali pendekezo la Marekani la kusitisha mapigano kati yake na Urusi kwa siku 30.
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amesema Marekani pia watajaribu kuishawishi Urusi kukubaliana na pendekezo hilo.
Hata hivyo, bila kutoa maelezo ya ziada Msaidizi wa ngazi wa juu wa Rais Zelensky amesema walijadiliana pia na maafisa wa Marekani juu ya dhamana za kiusalama kwa Ukraine.
Jitihada za Trump za kumaliza vita hivyo, tayari zinaonesha matumaini baada ya makubaliano hayo yaliyofanyika Jeddah, Saudi Arabia.