Johansen Buberwa – Kagera.

Shirika la Agrithaman kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa Global Alliance for Improved Nutrition (GAIN) linalojihusisha na masuala ya lishe wameandaa semina kuhusu salama wa chakula, ili kujenga uelewa kwa jamii.

Jumla ya washiriki 180 Bukoba Mjini wamehudhuria ambao ni viongozi wa soko kutoka kata  za Kashai, Rwamishenye, Bakoba Custom, Nyakanyasi na Soko Kuu, wawakilishi wa wauza nbogamboga, matunda na samaki.

Mkurugenzi wa Shirika la Agrithaman Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Neema Rugangira akifungua mafunzo hayo hii leo Machi 15, 2025 amesema yametokana na kufanya ziara katika masoko na kuona namna ambavyo wauzaji wa mboga mboga na vyakula vya nafaka wanavyohifadhi vyakula kwa njia zisizo salama.

“Lengo la mafunzo haya ni kuandaa mabalozi bora ambao wanaweza kutumika kuwafundisha wananchi wote namna nzuri ya kuhifadhi chakula na kujua ni kwa jinsi gani wananchi wanaweza kitambua chakula na matunda yaliyoribika ili yasitumike na kuondoka changamotoo za kiafya hasa kansa na vifo ndio maana tumechukua viongozi katika masoko yote ya Bukoba na viongozi wa kata zote 14,” amesema Lugangira.

Kwa upande wake ofisa wa Sera na chakula kutoka Shirika la  Kimataifa la GAIN, Reticia Ishengoma amesema wamefaya utafiti na kugundua kuwa Watanzania wanaopata magonjwa ya Kansa, yanayotoka na uhifadhi mbaya wa vyakula na wengi wao wanatokea Kanda ya Ziwa ikiwemo mkoa wa Kagera hivyo wanapaswa kuwa makini.

“Katika masoko matano ambayo nimeyapitia Bukoba mjini nimekuta baadhi ya wauzaji wa matunda na mboga mboga wakitumia dawa katika bidhaa na bidhaa hizo zikiendelea kuuzwa sokoni kuwa kuwa vyakula vingi vya Nafaka kama mahindi na Karanga vinavyouzwa sokono  vikohatarini kupata Sumu kuvu kwa asilimia kubwa kwani njia inayohifadhi bidhaa hizo sio salama,” amesema Reticia.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Bukoba, Proscovia Mwambi amesema kuwa kupitia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa kusaidia na viongozi mbalimbali kupitia mafunzo hayo wataweka utamaduni wa kutembelea  masoko na kutoa elimu kwa wananchi juu ya kutambua vyakula vilivyoharibika na jinsi ya kuhifadhi vyakula kwa usalama ili kujenga kizazi bora.

Mafunzo hayo yametoa fursa kwa washiriki kueleza changamoto za kuhifadhi vyakula na namna bora ya washiriki kufundishwa madhara makubwa yatokanayo na  matumizi ya vyakula ambavyo  havijahifadhiwa vizuri na jinsi ya kuepuka ikiwemo kuboresha lishe za watoto wao kupitia vyakula vyao.

Aidha, yalishirikisha Viongozi wa Serikali kutoka kwenye mitaa na kata zenye masoko, viongozi wanawake 2 wa mitaa yote maafisa kutoka manispaa wa idara za afya  lishe, kilimo, na mifugo ili kupata uelewawa pamoja kuhusu maswala ya usalama wa chakula.

Kamati yakoshwa ujenzi bora mwalo wa Chato Beach
Maisha: Siamini, yaani mdogo wangu kalala na mke wangu