Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini, Kwagilwa Reuben, amesema kuwa wabunge na wananchi wa ukanda wa kaskazini wanaunga mkono uamuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kununua umeme kutoka Ethiopia kupitia Kenya, kwani hiyo ni fursa ya maeneo ya kanda hiyo kuwa na vyanzo vya kutosha vya umeme.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo, Machi 16, 2025, Jijini Dodoma, ambapo amesema kuwa wanaopinga mpango huo hawana uelewa wa hali halisi ya mahitaji ya nishati nchini.
“Tanzania si nchi ya kwanza kununua umeme kutoka nje, kuna mataifa mbalimbali ambayo yanaunua umeme mfano kama Marekani, India, Afrika Kusini, na Kenya, hawa pia hununua na kuuza umeme kwa nchi jirani kutokana na jiografia na mahitaji yao ya nishati.

“Kwa mfano kama Mkoa wa Arusha hakuna chanzo chochote cha kuzalisha umeme na hata makaa ya mawe hawana, hakuna gesi, hakuna upepo wala maporomoko ya kuweza kuzalisha umeme, kwaio huamuzi wa kununua umeme kutoka ethiopia sisi watu wa ukanda wa kaskazini huo tunaona ni huamuzi wa msingi sana,” amesema Kwagilwa.
Amesema Kwa umeme wa Ethiopia wao watachukulia kupitia Namanga, ukiwa tayari umeshapita kwenye miundombinu ya Ethiopia na Kenya.

“Mita yetu kuu itakuwa Namanga, na baada ya Namanga utapelekwa moja kwa moja kwa Wananchi, Majumbani, Viwandani, Mashambani, migodini na sehemu nyingine na wananchi watalipa kulingana na matumizi (watalipa kwa Tariffs), tunanunua kwa senti saba ya dola, Dunia yote inafanya hivyo,” amesema.
“Tukiangalia wenzetu wananunua umeme kutoka Canada, Mexico na Jamaika,na sisi Tanzania tupo kwenye mazungumzo kuwauzia umeme Rwanda na Burundi”. Amesema Kwagilwa
Hata hivyo Mikoa ya Kaskazini ni
Mikoa ambayo inahitaji umeme wa Uhakika kwa kiasi kikubwa sana.

“Kaskazini ni kitovu cha utalii, Tanzania kuchukua umeme Ethiopia na kuleta kaskazini ni kuweka uhakika wa huduma kwa watalii wetu, lakini pia ni sehemu penye migodi mingi (Tanzanite, Graphile,Gold, Chumvi), Kaskazini pana viwanda vingi (Vinywaji, cement, mbolea, ngano)”,
“Kaskazini pana Mashamba makubwa ya Ngano, Kaskazino ipo Bandari ya Tanga ambayo yote hiyo inategemea kuendeshwa na umeme wa uhakika,” amesema Kwagilwa.