Waasi wa AFC – M23 wamesema hawatoshiriki mazungumzo ya amani yaliyoratohuwa na Angola, wakimtuhumu Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi kwa kuendeleza mapigano.
Taarifa ya M23 iliyotolewa Februari 17, 2025 katika chapisho la Mtandaoni, imeeleza kuwa Serikali ya DRC imekuewa ikiendesha mashambulizi ya ardhini kwa kutumia ndege za kivita.
Machi 17, Msemaji wa M23, Lawrence Kanyuka alisema wawakilishi wao wangesafiri kuelekea Luanda kwa ajili ya mazungumzo hayo, yaliyoratibiwa na Rais wa Angola, João Lourenço, baada ya kukutana na Rais Felix Tshisekedi.
Mazungumzo ya kutafuta suluhu kati ya Kongo na Rwanda yalivunjika Desemba 2024, baada ya Rwanda kuweka sharti la kufanyika mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Kongo na waasi hao wa M23.