Klabu ya Saudia Al-Nassr inapanga kutoa ofa ya kumnunua beki wa kati wa Arsenal na Brazil Gabriel Magalhaes, 27 msimu wa joto. (GiveMeSport)
Real Madrid wataongeza dau lao la kumsajili beki Dean Huijsen mwenye umri wa miaka 19 kutoka Bournemouth msimu huu wa joto baada ya kupandishwa kwenye kikosi cha wakubwa cha Uhispania. (Sun)
Bournemouth wanaongoza katika kinyang’anyiro cha kumsajili mlinda mlango wa Jamhuri ya Ireland Caoimhin Kelleher, 26, kutoka Liverpool. (Sportsport)

Chanzo cha picha,Getty Images
Newcastle United wanatayarisha ofa ya mkataba mpya ambao utaongeza maradfu mshahara wa mshambuliaji wa Sweden Alexander Isak, 25, (GiveMeSport).
Napoli watajaribu kumnunua mshambuliaji wa Denmark Rasmus Hojlund msimu huu wa joto, lakini hawawezi kumudu bei inayotakiwa na Manchester United ya £50m. (Gazzetta dello Sport)
Mshambulizi wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 26, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Galatasaray, anaweza kwenda Manchester United kama sehemu ya mkataba wa Hojlund kwenda Napoli (Mirro)
Chelsea wanafikiria kulipa ada ya adhabu ili kukwepa jukumu la kumnunua moja kwa moja kwa pauni milioni 25 kiungo Jadon Sancho msimu huu wa joto, ambaye yuko hapo kwa mkopo akitokea Manchester United. (The i paper)

Chanzo cha picha,Getty Images
Mkurugenzi mpya wa michezo mtarajiwa wa Arsenal Andrea Berta anavutiwa na mshambuliaji wa Wolves raia wa Brazil Matheus Cunha, ambaye ana kipengele katika mkataba wake cha kuuzwa kwa £62.5m. (Teamtalk)
Kiungo wa kati wa Ufaransa Eduardo Camavinga, 22, yuko tayari kujiunga na Manchester City msimu huu wa joto huku kukiwa na wasiwasi kuhusu nafasi yake katika kikosi cha kwanza cha Real Madrid. (Football Insider)
Kocha mkuu Unai Emery anaishinikiza timu yake ya Aston Villa kumsajili kw auhamisho wa kudumu mshambuliaji wa Hispania Marco Asensio, 29, anayetoka kwa mkopo Paris St-Germain. (GiveMeSport)
Arsenal wanafuatilia kwa karibu masuala ya mkataba wa Leroy Sane huko Bayern Munich kwani winga huyo wa Ujerumani, 29, anaweza kupatikana kwa uhamisho wa bure msimu huu wa joto. (Football Insider)
Kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo, 19, ni mmoja wa wachezaji ambao Manchester United wako tayari kuwauza msimu huu wa joto ili kuongeza bajeti yao ya uhamisho. (Florian Plettenberg)

Chanzo cha picha,Getty Images
Winga wa Ureno Bernardo Silva, 30, anatarajia kusalia Manchester City msimu huu wa joto ili kumalizia mkataba wake. (Mirror)
Tottenham ni moja ya vilabu kadhaa vinavyovutiwa na kiungo wa kati wa Inter Miami Mmarekani Benjamin Cremaschi, 20, ambaye ni mmoja wa wachezaji wanaopendwa sana na Lionel Messi (Teamtalk)
Barcelona wanataka kumuuza Ansu Fati, 22 msimu huu wa joto, ingawa winga huyo wa Hispania, alikataa kuuzwa katika dirisha lililopita la Januari. (Fabrizio Romano)
Manchester United ni moja ya vilabu kadhaa vya ligi kuu England vinavyofikiria kumnunua kiungo wa kati wa Sunderland Jobe Bellingham mwenye umri wa miaka 19. (Teamtalk)
Crystal Palace wanapanga mpango wa kumsajili mshambuliaji Muingereza Hayden Hackney mwenye umri wa miaka 22 kutoka Middlesbrough msimu huu wa joto. (Football Insider)