Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Nchini (THBUB), imewataka Wananchi wa Mkoa wa Manyara kufichua vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu ikiwemo unyanyasaji, rushwa pamoja na ukatili wa kijinsia, ili kutokomeza vitendo hivyo vinavyoathiri ustawi wa Wananchi katika nyanja za kijamii na kiuchumi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Mohamed khamis Hamad amesema kuna umuhimu wa jamii kutambua na kuziheshimu haki za binadamu.

Kwa upande wao Mchunguzi Mkuu Msaidizi, Halfan Rajab Botea na Mkurugenzi wa Idara ya Elimu kwa Umma, Mawasiliano, Utafiti na Nyaraka kutoka Tume ya Haki za Binadamu, Monica Laurent wamesema watatoa elimu kwa makundi ya Wananchi, Wanafunzi pamoja na vyombo vya sheria.

Tunatekelezaji mipango maalum huduma za kuchuja damu - MSD
Kamati ya Kudumu ya Bunge yaridhishwa na hatua za utekelezaji mradi wa Taza