Mamlaka ya mapato (TRA)  Mkoa wa Pwani imeendelea kutoa elimu ya umuhimu wa kulipa kodi kwa wananchi wa Mkoa huo lengo likiwa ni kuongeza mwitikio wa kulipa kodi kwa hiari na kukuza mapato.

Mpango huo ambao umepewa jina la Elimu ya kodi mlango kwa mlango pia unahusisha kuibua walipa kodi wapya ambao awali ama walikuwa wanafanyabishara zao bila kujua kuwa wanatakiwa kusajiliwa na wale waliokuwa wanatambua sheria lakini hawakuwa wanaifuata.

Hayo yamebainishwa Machi 25,2025 na Afisa mkuu msimamizi wa kodi kutoka (TRA) Charles Mkubwa wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa mpango huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon.

Baadhi ya maafisa wa Mamlaka ya mapato (TRA) wakiwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani wakitoa taarifa juu ya mwenendo wa utekelezaji wa llimu ya kodi mlango kwa mlando ambayo maafisa hao wameendelea kuitekeleza Mkoni humo.

“‘Tunawafikia walipa kodi tunawapa elimu na kuwafahamisha hasara wanazoweza kupata endapo wataendesha biashara zao bila kujisajili lakini pia tunawaeleza faida watakazopata iwapo wataingizwa kwenye mfumo”amesema.

Ametaja baadhi ya faida ambazo mfanyabishara anaweza kuzipata iwapo atasajili biashara yake ni pamoja na kupata mikopo kutoka kwenye taasisi za fedha na kutambulika kisheria.

“Mpango huu unatuwezesha kukutana na walipa kodi kwa urahisi tifauti na ule utaratibu wa kuwaalika kwenye semina unakuta wengi tunawakosa maana hawawezi kuja wote,” amesema.

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Nickson Simon amepongeza mpango huo na kusema kuwa utaongeza ufanisi wa utendaji wa kazi na kukuza mapato ya serikali.

“Hivi sasa bajeti ya Halmashauri ya Kibaha Mji kwa mwaka ni sh bilioni 47 lakini makusanyo ni bilioni 12 hivyo kila mwaka tunapata sh bilioni 35 kutoka serikaki kuu na hizi tunazipata kwakuwa watu wanalipa kodi hivyo nichukue nafasi hii kuwahimiza wananchi waendelee kulipa kodi”amesema.

Amesema kuwa ili kuhakikisha mpango huo unakamilika kwa ufanisi kuna umuhimu wa Mamlaka hiyo kushirikiana na mamlaka zingine ikiwemo halmashauri.

Neema Jackson Mkazi wa Kibaha amesifu mpango wa (TRA )kwa kuwatembelea walipa kodi na kuwapa elimu na kueleza kuwa utaratibu huo utaimarisha upendo na ushirikiano katika kuboresha mapato.

“Miaka mingi wananchi wamekuwa wakiwaona( TRA ) wanakuja wanawakimbia kwakua wanaamini kuwa wao ni kufunga maduka lakini kwa namna walivyoweka utaratibu huu mpya wananchi watajenga urafiki kwao,” amesema.

Maisha: Ananilazimisha kutoa mimba yake kisa ana mke
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Machi 26, 2025