Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) umejipanga kutoa vifaa vya TEHAMA katika Shule 22 huku ikisema pia umeingia mikataba ya kufikisha mawasiliano katika Kata 1,974 zenye vijiji 5,102 na Wakazi 29,193,753.
Akizungumza na Waandishi wa habari Leo Machi 27, 2025, Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo, Mhandisi Peter Mwasalyanda ambapo amesema Vifaa hivyo ni pamoja na TV, Mashine ya Braille (Nukta Nundu) Msomaji wa obiti (Machine za Kisasa), Kompyuta za mkononi, Printa ya nukta nundu, Rekoda za sauti za dijiti na Vikuzaji.
Amesema, kupitia mpango huo, jumla ya Minara 2,152 imejengwa na Miradi imekamilika,Kata 1,627 Zenye vijiji 4,482
Wakazi 24,640,304 Jumla ya Minara 1,783 imekamilika.
Amesema Serikali katika kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma za mawasiliano kwa kujenga minara 758 Nchi iliingia mikataba mwezi Mei 2023 na watoa huduma kwa ajili ya kufikisha mawasiliano maeneo ya vijijini.
“Mradi huu wa ujenzi wa minara 758 ni mradi mkubwa kuwahi kutekelezwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mradi huu ni wa kimkakati ni utafikisha mawasiliano kwenye Kata 713 Kunufaika“, amesema.
“Wilaya 127 Kunufaika, Mikoa 26 kunufaika, Wananchi 8.5M watafikiwa na huduma za uhakika za mawasiliano na Ruzuku TZS 126Bn kutumika”. Amesema Mhandisi Mwasalyanda
Amesema Hadi kufikia tarehe 24 Machi 2025 minara 430 imejengwa na kuanza kutoa huduma kwa wananchi wa maeneo ya vijiji.