Chama cha Mapinduzi ( CCM), Kimezindua Kampeni zake katika Jimbo la Dimani Mkoa wa Mjini Magharibi huku kikishangaa CUF kwa  kushindwa kutanua wigo wa demokrasia ndani ya Chama hicho na kuendelea kumshikilia  mgombea mmoja  wa kudumu  miaka kwa miaka.

Kimesema kuwa watu wataendelea kukichagua CCM kwa sababu ya kufuata misingi bora ya ya demokrasia,misimamo thabiti,sera endelevu  na utaratibu wake wa kubadili wagombea.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa chama hicho Abdulrahman Kinana alipokuwa akizindua kampeni za CCM zilizofanyika Maungani nje kidogo ya mji wa Unguja,amesema kuwa CCM itaendelea kuchaguliwa na wananchi kwa sababu kinatimiza wajibu wa kuwatumikia wananchi, kutimiza matakwa ya kisera na kushughulikia matatizo na shida za wananchi.

”Kuna mgombea mmoja hapa Zanzibar ameanza kugombea urais tokea akiwa na miaka 30 sasa ana miaka 80,toka akiwa kijana mbichi sasa amekuwa kikongwe na kupinda mgongo ila bado ana tamaa ya kuwania urais” amesema Kinana.

Aidha, Kinana amewashangaa wanachama wa CUF ambao wanakubali kudanganywa  kirahisi kila siku na kuaminishwa kwamba ipo siku mgombea wao wa urais aliyeshindwa uchaguzi atatangazwa na Umoja wa Mataifa kuwa rais wa Zanzibar.

Hata hivyo,Kinana amewaomba  wananchi wa Dimani kumchagua mgombea ubunge aliyesimamishwa kwa tiketi ya CCM,Juma Ali Juma kwa sababu ni makini,mchapakazi na mwepesi wa kuwatumikia wananchi.

Arsenal Yapata Majanga, Viungo Wawili Wasalia Kikosi
Riyad Mahrez Mchezaji Bora Barani Afrika