Kiungo mshambuliaji wa mabingwa wa soka nchini England Leicester City, Riyad Mahrez ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika mwaka mwaka 2016.

Mahrez ambaye ni raia wa nchini Algeria, alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo katika hafla maalum iliyoandaliwa na shirikisho la soka barani Afrika CAF mjini Abuja nchini Nigeria, usiku wa kuamkia hii leo.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, ameshinda tuzo hiyo huku akiwazidi wapinzai wake Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon, Borrusia Dortmund) na Sadio Mane (Senegal, Liverpool) kwa kupata kura 361.

Msimu uliipita Mahrez alikua chachu ya kuiwezesha klabu ya Leicester City kutwaa ubingwa wa soka nchini England, huku akifunga mabao 17.

Wakati huo huo kiungo mshambuliaji wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Nigeria Alex Iwobi, ametangazwa kuwa mchezaji bora wa Afrika mwenye umri mdogo.

Kwa upande wa tuzo ya mchezaji bora wa kike barani Afrika kwa mwaka 2016, imekwenda kwa mwanadada kutoka nchini Nigeria Asisat Oshoala.

Tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2016 kwa wanaocheza barani Afrika imekwenda kwa mlinda mlango kutoka nchini Uganda na klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika kusini Denis Onyango.

Kocha wa klabu ya Mamelodi Sundowns Pitso Mosimane, ambaye alikiwezesha kikosi chake kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Afrika, ametangazwa kuwa kocha bora wa mwaka 2016.

Bakary Papa Gassama ametangazwa kuwa mwamuzi bora wa mwaka 2016.

Katika picha ni kikosi bora cha mwaka 2016 cha barani Afrika.

Image result for Mahrez Is Africa’s Best Footballer In 2016

Kinana asema CCM itaendelea kushinda chaguzi zote
John Obi Mikel Atimka Stamford Bridge