Wakati sheria ya Usalama barabarani inamtaka kila dereva wa bodaboda kuwa na kofia ngumu (halmeti) mbili kwa ajili yake na abiria wake, watumiaji wa kofia hizi wapo hatarini kuambukizwa maradhi ya ngozi.
Athari hiyo inatokana na helmeti chafu, ambapo baadhi ya waendesha bodaboda walieleza na kukubaliana na tatizo hilo, helemti ni chanzo cha magonjwa ya ngozi kutokana na kutumiwa na abiria mbalimbali bila kufuliwa kwa muda mrefu na dereva inamuwia vigumu kufua kofia hiyo kutokana na sheria zinazombana dereva akiwa barabarani ambapo ufuaji wa kofia humchukua siku tatu kukauka hali ambayo si salama pale anapokuwa barabarani kupambana na sheria za usalama barabarani.
Mganga Mkuu Mkoa wa Dodoma, Dk. James Kiologwe alisema watumiaji wa usafiri huo wamekuwa wakitumia helmeti moja bila kujali kama imefanyiwa usafi. huku wengine wakilazimika kuvaa chafu ili kutekeleza matakwa ya sheria.
Pia Daktari alitaja magonjwa ya fangasi za kichwa, chawa ni rahisi sana kuambukiza japo alikazia kufanyika utafiti zaidi kujua athari nyingine za kushiriakiana kofia hizi.
Daktari hakuishia hapo aliweza kutoa suluhisho juu ya hili, alishauri kila abiria ni vema kuwa na kitambaa ambacho atajifunga kichwani kabla hajavaa kofia ili kuzuia kofia hiyo moja kwa moja kugusa kichwa na kupunguza makali ya kusambaa kwa magonjwa hayo kirahisi.
Tatizo hilo limekuwa sugu kiasi ambacho inawapelekea waendesha bodaboda kukosa abiria kutokana na uchafu wa helmeti zao, baadhi ya madereva bodaboda walitoa maoni kwamba ipitishwe sheria, kila abiria mabaye shughuli zake zinajihuisha na utumiaji wa usafiri wa pikipiki awe na kofia yake ili kuepuka kushirikiana utumiaji wa kofia hizo ngumu kwa ajili ya usalama wa barabarani na kumuepusha na magonjwa yatokanayo na kushirikiana kofia hiyo.