Kitendawili cha kutangazwa kwa mchezaji bora wa dunia wa FIFA kitateguliwa hii leo kwenye hafla maalum ambazo zitafanyika mjini Zurich nchini Uswiz.

Kwa saa za Afrika mashariki hafla ya utoaji wa tuzo hiyo itaanza mishale ya saa mbili na nusu (2:30) Usiku.

Tuzo hiyo inajulikana kwa jina la “THE BEST FIFA FOOTBALL AWARD” na hii ni baada ya kutengana na zile za Ballon D’or.

Mbali na tuzo ya mchezaji bora upande wa wanaume, pia washindi wa tuzo nyingine watatangazwa katika hafla za hii leo, na ifuatayo ni orodha ya walioteuliwa kuingia fainali.

Mchezaji Bora wa Kiume

Washiriki: (•Cristiano Ronaldo •Antoine Griezmann •Lionel Messi)

 

Mchezaji Bora wa Kike

Washiriki: (•Melanie Behringer •Carli Llyod •Marta)

 

Kocha Bora wa Kiume

Washiriki: (•Claudio Ranieri •Fernando Santos •Zinedine Zidane)

 

Kocha Bora wa Kike

Washiriki: (•Jill Ellis •Sulvia Neid •Pia Sundhage)

 

Goli Bora la Mwaka 2016

Washiriki: (•Marlone •Deniuska Rodriguez •Mohd Faiz Subri)

 

Tuzo ya Fair Play

Tuzo ya Mashabiki Bora

Washiriki: (•ADO Den Haag Supports •Borussia Dortmund-Liverpool Supports •Iceland Supports)

Meneja wa Young Dee azungumzia taarifa za rapa huyo kuurudia ‘Unga’
RC Rukwa atoa agizo kwa wakuu wa wilaya kuhusu mifugo