Uongozi wa FC Barcelona umempiga marufuku Lionel Messi kuhudhuria hafla ya utoaji wa tuzo kwa mchezaji bora wa dunia wa FIFA itakazofanyika mjini Zurich nchini Uswiz leo usiku.
FC Barcelona wametangaza marufuku hiyo kwa Messi, kwa kutaka kutoa nafasi kwa meneja Luis Enrique kuwa na kikosi chake chote katika maandalizi ya mchezo wa mkondo wa pili wa kombe la Mfalme dhidi ya Athletic Bilbao.
Katika mchezo wa mkondo wa kwanza FC Barcelona walikubali kupigwa mabao mawili kwa moja.
Messi yupo katika orodha ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa FIFA kwa mwaka 2016, sambamba na Cristiano Ronaldo na Antoine Griezmann.
#FCBlive Consulta el comunicado del FC Barcelona sobre la Gala The Best FIFA Awards https://t.co/v7jg17TqMC pic.twitter.com/SF7soICUGt
— FC Barcelona (@FCBarcelona_es) January 9, 2017
Ronaldo anapewa nafasi kubwa ya kutangazwa mshindi wa tuzo hiyo, kutokana na kigezo cha kuwa na msimu mzuri kwa mwaka 2016, ambapo aliisaidia Real Madrid na timu yake ya taifa ya Ureno kutwaa ubingwa wa Ulaya huku akitwaa ubingwa wa dunia upande wa klabu.
Tayari mshambuliaji huyo ameshamgaragaza Messi katika tuzo Ballon d’Or, ambapo mshindi walitangazwa mwezi Disemba mwaka 2016.