Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo ametangazwa kuwa mchezaji bora wa dunia wa FIFA kwa mwaka 2016.
Ronaldo alitangazwa kuwa mfalme wa tuzo hiyo, usiku wa kuamkia hii leo katika hafla maalum zilizofanyika mjini Zurich nchini Uswiz.
Ronaldo amewashinda wapinzani wake ambao waliingia tatu bora, Lionel Messi wa FC Barcelona na mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann.
Mshambuliaji huyo ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Ureno, anaweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa FIFA, baada ya shirikisho hilo kuvunja ushirika na waratibu wa tuzo za Ballon d’Or.
Tuzo ya mchezaji bora wa kike imekwenda kwa mwanadada kutoka nchini Marekani Carli Lloyd ambaye anaitumikia klabu ya Houston Dash.
Kwa upande wa tuzo nyingine matokeo yalikua kama ifuatavyo.
Kocha Bora wa Kiume
Claudio Ranieri
Kocha Bora wa Kike
Sulvia Neid
Goli Bora la Mwaka 2016
Mohd Faiz Subri.
Tuzo ya Fair Play
Klabu ya Atletico Nacional ya nchini Colombia
Tuzo ya Mashabiki Bora
Liverpool Supports