Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi imekataa ombi la kuingia ubia na shule za binafsi kwa madai kuwa Serikali ina shule za kutosheleza mahitaji yaliyopo na haihitaji msaada kutoka shule binafsi katika kukabiliana na changamoto zilizopo katika suala la vyumba vya madarasa.

Aidha ombi hilo limeombwa na mameneja wa shule na vyuo visivyo vya serikali (Tamongsco), wamiliki hao wameiandikia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi kuiomba iwashirikishe katika udahili wa wanafunzi 12,000 ambao wamefaulu mtihani wa darasa la saba mwaka jana, lakini kutokana na ukosefu wa madarasa  hawataweza kwenda kidato cha kwanza.

“Kila mwaka tunaiomba serikali ituondolee kodi, badala yake shule binafsi zipewe ruzuku ili watoto wanaokosa nafasi za kusoma katika shule za serikali kila mwaka wapate elimu hiyo katika shule binafsi kwa mikataba maalumu ya ubia wa sekta ya umma na binafsi,”amesema Katibu Mkuu wa Tamongsco Benjamin Nkonya.

Kwa upande wa Serikali kupitia  kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Profesa Msanjila, amesema kuwa Serikali imeamua kuboresha shule zake na kutoa elimu bure, jambo ambalo limewavutia wananchi wengi kupeleka watoto wao katika shule za serikali tofauti na miaka ya nyuma.

“Hawa tulitaka kuweka ada elekezi, lakini walitumia wanasiasa kupinga, kwa madai kuwa tunaingilia elimu ambayo serikali haihusiki, jambo hilo serikali imeamua kuachana nalo ili soko liweze kuamua,”amesema Prof. Msanjila.

FIFA Kuongeza Timu Shiriki Fainali Za Kombe La Dunia
Kiti Cha Arsene Wenger Chamtesa Roberto Mancini