Aliyekuwa meneja wa klabu ya Man city Roberto Mancini ana ndoto za kumrithi Arsene Wenger.

Mancini ameonyesha hali hiyo kwa kueleza kuwa, anasubiri kuoona ama kusikia taarifa kutoka wa viongozi wa Arsenal kuhusu wito wa kuchukua nafasi ya umeneja klabuni hapo.

Taarifa zilizochapishwa na TMW zimeibua siri hiyo ya Mancini, ambaye anaamini Wenger atatangaza kuondoka Arsenal itakapofika mwezi Februari, huku akisubiri kumalizia mkataba wake mwishoni mwa msimu huu.

Mtaliano huyo ana matumaini makubwa ya kuwa sehemu ya watakaopewa nafasi ya kuchukua nafasi ya Wenger, kwa kudai falsafa za ufundishaji wake zinataka kufanana za mzee huyo kutoka nchini Ufaransa.

Tayari Mancini ambaye pia aliwahi kukinoa kikosi cha Inter Milan kwa nyakati mbili tofauti, ameshakataa ofa ya kufundisha soka nchini China, kwa kuamini bado ana nafasi ya kuelekea kaskazini mwa jijini London.

Akiwa Man City, Mancini alifanikiwa kutwaa ubingwa wa England msimu wa 2011–12, FA Cup msimu wa 2010–11 pamoja na ngao ya jamii (FA Community) 2012.

Serikali yashtukia mtego wa shule binafsi
Jürgen Klopp: Coutinho Haendi Popote