Wajumbe wa baraza kuu la Shirikisho la Soka Duniani FIFA hii leo wanatarajiwa kupiga kura zitakazoamua mpango wa kuongeza timu shiriki katika fainali za kombe la dunia kutoka 32 hadi 48.

Mpango huo ukiidhinishwa, utaanza kutumika wakati wa fainali ekelezwa Kombe la Dunia la 2026, na utafaidisha mabara ya Afrika na Asia.

Mpango huu umekuwa ukipigiwa debe na rais wa shirikisho hilo Gianni Infantino tangu akiwa katika kampeni za kuwani kiti cha urais.

Iwapo mpango huo utaidhinishwa, itakuwa mara ya kwanza kwa fainali za Kombe la Dunia kuongezewa timu tangu mwaka 1998.

Kuna mapendekezo matano ambayo baraza kuu la FIFA lenye wanachama 37 litaangazia.

  • Kombe la Dunia lenye timu 48 na makundi 16 ya timu tatu kila kundi ambapo timu mbili bora zitasonga kwa hatua ya mtoano ya timu 32 (mechi 80 kwa jumla).
  • Kombe la Dunia la timu 48, mechi moja ya muondoano wa kufuzu ambapo mshindi atajiunga na timu 16 nyingine (mechi 80 kwa jumla – 16 za mtoano wa kufuzu na 64 za michuano kamili).
  • Kuwa na timu 40 na makundi 10 ya timu nne kila kundi ambapo mshindi, na timu sita pekee zitakazomaliza namba mbili katika kila kundi ndizo zitafuzu (mechi 76).
  • Kuwa na timu 40 na makundi manane ya timu tano kila kundi (mechi 88).
  • Kusalia na Kombe la Dunia lilivyo sasa ambapo kuwa timu 32 (mechi 64).

Infantino mwenye umri wa miaka 46, ambaye alimrithi raia mwenzake kutoka nchini Uswiz Sepp Blatter kama rais wa FIFA mwezi Februari 2016 alifanya kampeni akiahidi kuongeza idadi ya timu kwenye michuano hiyo.

Awali alipendekeza ongezeko la timu na kufikia 40, wazo lililowasilishwa na rais wa wakati huo wa Uefa Michel Platini 2013, kabla ya kubadilisha msimamo na kuunga mkono michuano ya timu 48.

Chini ya mpango wa Infantino anaoupendekeza kwa sasa, mechi zinaongezeka kutoka 64 hadi 80, lakini fainali bado zinaweza kuchezwa kwa kipindi sawa na cha sasa cha siku 32.

Timu yoyote shiriki haitatakiwa kucheza zaidi ya mechi saba, sawa na ilivyo chini ya mpango wa sasa.

Udhaifu pekee ni kwamba huenda mikwaju ya penalti ikatakiwa kutenganisha timu shiriki zitakazotoka sare kwenye hatua ya makundi.

Milanzi: Tutahakikisha tunatokomeza ujangili
Serikali yashtukia mtego wa shule binafsi