Aliyekuwa mgombea urais wa Chadema  na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa amesema amesikitishwa na vyama hivyo  baada ya kila chama kusimamisha mgombea kuwania Udiwani Kata ya Matevesi, Wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha.

Amesema kuwa hali hiyo inaweza kuwanyima ushindi wagombea wa vyama hivyo dhidi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho kinaonekana kuwa na nguvu.

Aidha vyama hivyo vilivyomo ndani ya Ukawa vilivyosimamisha wagombea  katika Uchaguzi huo ni Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi, Lowassa amesema vyama hivyo vimefanya kosa la kiufundi linaloweza kusababisha  kuanguka katika uchaguzi huo na kuonya kuwa makosa kama hayo yasijirudie tena.

“Nyie mmefanya makosa makubwa ya kiufundi kwa kila chama ndani ya Ukawa kusimamisha mgombea wake, hapo ndipo CCM wanaposhindia kwa hiyo pigeni kampeni za nguvu ili mshinde,”amesema Lowassa.

Kwa upande wake Katibu wa siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Arusha Shaaban Mdoe, amesema kuwa kauli hiyo ya Lowassa ni utabiri mzuri wa ushindi wa Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi huo.

 

Video: Obama atoa hotuba yake ya mwisho kama Rais, asisitiza demokrasia
AY: Ben Pol ndiye R.Kelly wetu Afrika