Beki wa pembeni wa Man Utd Luke Shaw anakabiliwa na wakati mgumu wa kumshawishi meneja wa klabu hiyo Jose Mourinho, ili kuepuka kimbunga cha kuondoshwa klabuni hapo.
Shaw anakabiliwa na janga la la kurejea katika kiwango chake cha soka, tangu alipoanza kucheza mwezi Novemba mwaka 2016 baada ya kupona jeraha ya kuvunjika mguu.
Meneja wa Man Utd Jose Mourinho amepanga kupunguza wachezaji ambao hawakidhi kwenye mipango yake katika kipindi hiki, kwa kigezo cha kuangilia kiwango na uwajibikaji klabuni hapo.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 21, atalazimika kutoa ushawishi wa kurejea katika kikosi cha kwanza kwa kukabiliana na wachezaji wenzake kama Daley Blind, Matteo Darmian na Marcos Rojo.