Msanii nyota wa Hip Hop, Abrahman Chande ambaye alikuwa akijulikana kama Dogo Janja na sasa akijiita ‘Janjaro ‘ , anayetamba na kibao chake cha kidebe wimbo uliofanya vizuri sana 2016.
Ameweka wazi na kuangushia lawama zake kwa maamuzi aliyoyafanya kuhusiana na kutoendelea kusoma kutokana na sababu za kimuziki, amefichua ya kwamba, kitu ambacho anajutia katika maisha yake ni kutoendelea na shule.
Akizungumza Dar es salaam jana, nyota huyo alisema aliamua kuachana na shule baada ya kuingizwa katika kundi la Tip Top Connection, ambapo alihakikishiwa maisha mazuri katika muziki.
”Mimi kitu ambacho mpaka leo huwa najutia ni kukosa shule kipindi ambacho ndio nimetoka Tip Top Conection, nilirudi Arusha halafu ndio nilikuwa nipo ‘form two’ halafu muda wa mitihani ulikuwa imekaribia pia ya ‘mock’, kwa hiyo wenzangu walifanya lakini mimi sikupata nafasi ya kujiandaa vizuri kwa ajili ya mitihani,” amesema Dogo Janja.
”Halafu nikakaa sana Arusha, nimerudi kama wiki tatu tu mtihani huu hapa, kwa hiyo nilifeli, hata kufeli kwangu hakukuwa kwa alama kubwa japokuwa niliweza kupitwa na vitu vingi ,”.
Dogo Janja alikuwa anasoma kwenye Shule ya Makongo ambapo alishindwa kuendelea mara baada ya kushindwa kufikisha alama za kumfanya aweze kuendelea kidato cha tatu katika shule hiyo.