Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, amewaagiza wananchi wanaoua tembo, watiwe mbaroni mara moja na kuchukuliwa hatua kali za kisheria bila kuonewa huruma.
Ametoa agizo hilo katika ziara yake ya kikazi ya siku tano katika Wilaya ya Karatu, aidha amewataka wananchi wanaoishi jirani na Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara pamoja na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kuacha mara moja tabia ya kushiriki tabia ya kushiriki katika ujangili.
“Mkuu wa polisi wa Mkoa pamoja na mkuu wa polisi wa Wilaya ya Karatu,wakamateni wananchi wote wanaojihusisha na vitendo vya na wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria,” amesema Gambo.
Gambo amesema kuwa Serikali haiko teyari kuona nyara zake zinazoingiza fedha nyingi nchini, zikiharibiwa na wananchi wasiokuwa na mapenzi mema na nchi yao.
Hata hivyo amewataka wananchi hao kufuata sheria za nchi na kuwaonya kuacha mara moja tabia hiyo ya kujihusisha na vitendo vya ujangili.