Katika kuhakikisha Mpira wa Miguu hapa Tanzania unasonga mbele, Kampuni ya Simu ya Airtel kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), wamezindua kliniki ya Airtel Rising Stars ya vijana 65 ambapo wavulana ni 40, huku wasichana wakiwa 25, ambao watachaguliwa kuingia katika timu za Kili Queens na Serengeti boys ambazo zitachaguliwa kuwakilisha nchi katika mechi za kimataifa.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Betrice Mallya, alipokuwa katika uzinduzi huo, amesema kuwa Kampuni ya Airtel inajitahidi kujenga misingi imara katika kuinua mpira wa miguu hapa nchini na kuibua vipaji vitakavyo saidia timu ya taifa.
Aidha, Mallya amesema ufunguzi wa Kliniki hiyo ni mafanikio makubwa kwa Kampuni hiyo kwani wanajenga msingi imara katika kuinua mpira wa miguu hapa nchini na ameomba makampuni mengine kuunga mkono juhudi hizo ili mpira wa miguu wa vijana uweze kusonga mbele.