Kiungo Yaya Toure amekataa ofa ya klabu ya Shanghai SIPG ya nchini China ambayo imeonyesha nia ya kumsajili na kumlipa mshahara mnono.

Toure amekataa ofa hiyo na kuweka wazi nia yake ya kutaka kuendelea kuitumikia klabu ya Man City ambayo ilimsajili mwaka 2010 akitokea FC Barcelona.

Shanghai SIPG imeonyesha kuwa tayari kumlipa mshahara kiungo huyo kutoka nchini Ivory Coast wa Pauni milioni 22.3 kwa mwaka ambapo kwa mtawanyiko wa malipo ya kila juma ni Pauni 430,000.

Mbali na kukataa ofa hiyo, taarifa nyingine zinadai kuwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33, aliwahi kuiweka kapuni ofa ya klabu ya Jiangsu Suning ya nchini China wakati wa dirisha dogo la usajili mwaka 2016.

Klabu hiyo ilijinasibu kumlipa Yaya Mshahara wa Pauni 520,000 kwa juma.

Kufuatia msimamo huo wa Toure, wakala wake Dimitri Seluk amesema: “Yaya anahitaji kucheza katika kiwango cha juu tena katika klabu zenye ushindani mkubwa duniani. Kwa sasa ana furaha akiwa na Manchester City, anapenda soka, hivyo maamuzi nayoyafanya ni sahihi kwa upande wake na wala haangalii sana fedha.”

Kwa sasa Toure anapokea mshahara wa Pauni 240,000 kwa juma.

Cristiano Ronaldo Amkataa Paulo Dybala
Mohamed Aboutrika Atuhumiwa Kwa Ugaidi