Mustakabali wa Lionel Messi wa kusaini mkataba mpya na FC Barcelona umeingia dosari, baada ya shughuli za kukamilisha suala hilo kufanywa kuwa siri.
Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa, uongozi wa FC Barcelona umeona kuna umuhimu wa jambo hilo kuendeshwa kimya kimya ili kutoa nafasi kwa kila upande kujiridhisha, kabla jamii kufahamishwa kwenye itakapofika hatua ya mwisho.
Tayari uongozi wa klabu hiyo ya Cataluña umeshakutana na kuafikia suala hilo, na wanaamini njia hiyo itakua salama zaidi kuliko ilivyokua hapo awali, ambapo baadhi ya mambo yaliwekwa wazi.
Maamuzi hayo yamefikiwa, kufuatia hofu iliyoligubika soka la barani Ulaya kwa sasa, ambapo uwekezaji mkubwa katika soka la China umekua kichocheo cha kuwavuta wachezaji wengi kimaslahi.