Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amesema kuwa mkoa wake hauna njaa baada ya kufanya ziara katika maghala mbalimbali ya wajasiriamali pamoja na kiwanda cha Unga cha Energy Mills vyote vilivyopo katika mji wa Sumbawanga.

“Mmejionea wenyewe, Katika Manispaa ya Sumbawanga suala la kwamba hakuna chakula ama kuna njaa ni maneno hewa, hakuna kitu kama hicho, Chakula kipo cha kutosha nafaka karibu zote zipo,” – Zelote Stephen.

Ameongeza kuwa wakulima wengi wameonekana kuuza mazao yao kwa wachuuzi na kusababisha wafanyabiashara wa masokoni kwenda kununua mazao hayo kwa bei nafuu ili wapate faida kisha wanaongeza bei jambo linalosababisha wananchi kushindwa kununua na wao kulalamika kuwa hakuna wateja.

Katika suala la malalamiko ya wananchi kuosa pesa Zelote Stephen alifafanua “malalamiko yaliyokuwepo kuwa pesa hakuna, nami nakubali, kipindi hiki tulichopo ni wakati wa kilimo na wakati wa kilimo maana yake kila mtu yupo shambani, na mwezi ujao (Februari) kuanzia tarehe 20, kuna taarifa kwamba watu wataanza kuvuna maharage, kwahiyo ni dhahiri kwamba suala la njaa na bei hakuna mtu ambae atalizungumzia.”

 

Cheyo: Wanasiasa msikurupuke kutangaza baa la njaa
Video: Majaliwa aagiza mkoa wa Mtwara kuchunguzwa