Shirika la Maendeleo ya Vijana nchini limepanga mikakati ya kupambana na kupunguza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini na kuongeza kuwa tatizo hilo limekuwa kubwa hasa kwa vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa.

Hayo yamesemwa na Mratibu Mwandamizi wa Miradi kutoka Shirika la Maendeleo ya Vijana nchini, Osca Kimaro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam, amesema kuwa vijana wengi wanajiingiza kwenye ngono wakiwa chini ya umri wa miaka 15.

Amesema kuwa tatizo hilo linazidi kuwa kubwa kila kukicha, hivyo wameamua kushirikiana na Serikali kwa kubuni mikakati ya kuweza kupunguza ongezeko la maambukizi ya Ukimwi kwa vijana.

Aidha, amesema lengo kubwa la kubuni mkakati ni kutaka kuwaondoa vijana katika tatizo hilo la maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwani vijana ndio nguvu kazi ya Taifa.

Hata hivyo amesema kuwa sababu kubwa ya inayowafanya vijana kuingia kwenye changamoto hiyo ni pamoja na kukosa taarifa sahihi za mahali ambapo huduma zinapatikana, huku akisema kuwa shirika hilo limepanga mkakati kuanzia mwaka 2015 mpaka 2020 kwaajili ya kuwasaidia vijana, ili waweze kuondokana na tatizo hilo.

Video: Walichosema ACT-Wazalendo kuhusu njaa,wasema CCM imepoteza nafasi yake
Serikali kuwaandaa vijana kushiriki uchumi wa viwanda