Chama cha ACT-Wazalendo, kimesema kuwa kuna uhaba mkubwa wa chakula hapa nchini kitu ambacho kinapelekea kutokea baa la njaa na kuongeza kuwa akiba iliyopo ni tani 90 tu, kulingana na taarifa ya BoT.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Itikadi na Mawasiliano wa chama hicho, Ado Shaibu, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari, amesema kuwa katika maghala ya chakula ya taifa kuna tani elfu 90 tu, kitu ambacho kinaashiria kuwepo kwa baa la njaa.

Aidha, Shaibu amemtolea mfano Mkuu wa Wilaya ya Longido kuwa amejitokeza na kusema ana uhaba wa chakula na anahitaji msaada wa haraka ili kuweza kunusuru hali hiyo.

Hata hivyo Shaibu amesema kuwa wanachokisema ni cha kweli hivyo wanataka kuchukua hatua ili waweze kuwaokoa watanzania wanaokabiliwa na baa hilo la njaa.

AFCON 2017: Cameroon Waongoza Kundi A
Video: Shirika la vijana kupunguza maambukizi ya virusi ukimwi