Bosi wa kikosi cha Crystal Palace Sam Allardyce, ameushangaza umma wa wapenda soka nchini England kufuatia mipango ya kutaka kumsajili beki wa pembeni kutoka nchini Wales Ben Davies.

Big Sam amejipanga kufanya usajili wa beki huyo kutoka Tottenham Hotspurs kwa ada ya uhamisho wa Pauni milioni 10.

Davies huenda akaondoka White Hart Lane, kutokana na hitaji lake la kutaka kucheza kila mwishoni mwa juma katika kikosi cha kwanza, na katika kipindi chote alichokaa klabuni hapo amekua chagulo la pili.

Mipango ya kujiunga na Crystal Palace imeibuka kwa mchezaji huyo, kufuatia mkakati wa uhamisho wake wa kuelekea Stadium Of Light yalipo makao makuu ya klabu ya Sunderland kushindikana.

Davies alitegemewa kujiunga na Sunderland, endapo beki wa pembeni wa klabu hiyo Patrick van Aanholt angeuzwa siku kadhaa zilizopita, lakini mmiliki Ellis Short alikataa kufanyika kwa dili hilo.

Hata hivyo Big Sam huenda akakabiliwa na upinzani wa kukamilisha dili la usajili wa Davies, kutokana na hitaji la Spurs la kutaka kumtumia kwenye michezo ya Europa League kuanzia mwezi ujao.

Pendekezo la kutafakari kuuzwa ama kutokuuzwa kwa Davies, limetolewa na mtendaji mkuu wa Spurs Daniel Levy ambaye anahofia kuanza kuingia sokoni kumsaka mbadala wake, kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili.

Nyota Airtel Watawala Ligi Ya Wanawake, Mechi Mbili Kuchezwa Kesho
Guangzhou Evergrande Wamtengea Mshahara Mnono Arda Turan