Timu ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume  ya Mipango imefanya ziara katika Kiwanda cha Tanga Cement kilichopo Mkoani Tanga ikiwa na lengo la kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na kiwanda hicho.

Akiwa katika eneo linalochimbwa mawe ya kutengenezea saruji, Kaimu Katibu Mtendaji kutoka Tume ya Mipango, Florence Mwanri amesema kuwa kiwanda hicho kina wajibu wa kuhakikisha sheria  na taratibu za utunzaji wa mazingira zinazingatiwa muda wote ili kuhakikisha mazingira yanabaki salama licha ya shughuli za uchimbaji kuendelea kufanyika.

Aidha,Mwanri ameupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kuendelea kutekeleza majukumu yake katika kuunga mkono dhamira ya Serikali ya kuwa nchi ya Viwanda na kuharakisha malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo inayosisitiza kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Kwa upande wake, Meneja wa Kiwanda hicho, Mhandisi Ben Lema amesema kuwa kiwanda hicho kimeendelea  kutoa ajira kwa watanzania katika kada mbalimbali ambapo kwa sasa kuna ajira zaidi ya 600 ambapo ajira 300 ni za moja kwa moja huku ajira 300 zingine ambazo sio za moja kwa moja zinajumuisha wauzaji, wasambazaji na wasafirishaji.

 

DC Iringa aagiza msako kwa waliofaulu na kutokwenda shuleni
JPM afanya uteua mabalozi watano